Kampuni ya Udalali ya YONO imetangaza tena zoezi la uuzwaji wa nyumba zinazomilikiwa na Kampuni ya Lugumi Enterprises baada ya zoezi hilo kushindikana hapo awali September tisa mwaka huu baada ya kukosekana mteja kwa kiwango kilichotakiwa.
Uuzwaji wa nyumba hizo unatokana na mmiliki wake Kampuni ya Lugumi Enteprises kudaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania deni ambalo serikali inataka lifidiwe kwa kuuzwa nyumba hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa YONO, Scolastika Kevera amesema zoezi la uuzwaji nyumba hizo sasa litafanyika Novemba tisa mwaka huu.
Mnada wa awali wa nyumba hizo ulifanyika Septemba 9, mwaka huu ambapo nyumba ya mfanyabiashara huyo iliyoko Upanga iliuzwa kwa shilingi milioni 700.
Mfanyabiashara huyo anadaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA), takribani shilingi bilioni 14 ambapo Kampuni ya Udalali ya Yono ndiyo iliyopewa kazi ya kupiga mnada nyumba hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scholastica Kevela, amesema leo kuwa serikali iliamua kufanya tathmini upya ili kupata thamani halisi ya nyumba hizo kazi ambayo tayari imekwishakamilika na zitauzwa upya huku thamani yake ikiongezeka lakini bei elekezi zitaletwa na TRA siku ya mnada.
“Tutaanza kuuza nyumba mbili zilizopo Mbweni JKT Wilaya ya Kinondoni zenye ukubwa wa mita za mraba 1,500 kila moja moja iliyopo Upanga yenye ukubwa wa mita za mraba 400, nyumba zote ni za kifahari ambazo zinafaa kwa matumizi ya ofisi na makazi hivyo, tunawakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi waje kununua,” amesema.
Mfanyabiashara huyo kupitia Kampuni yake ya M/S Lugumi Enterprises aliwahi kuingia katika uchunguzi na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambapo mwaka 2011 kampuni yake iliingia mkataba na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukulia alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya shilingi bilioni
0 comments :
Post a Comment