Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Musukuma amefunguka na kusema kuwa endapo wakishinda kesi dhidi ya mgodi wa GGM ambayo wamefungua wanaukika kupata fedha ambazo zinaweza kuhudumu katika halmshauri kwa miaka 29, bila kuomba kwa Rais fedha.
Musukuma amesema hayo alipokuwa kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya ya Geita ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wa CCM wote ambao wanahitajika kituo cha polisi waende polisi wenyewe wakahojiwe na kuwaambia siku ya kwenda mahakamani wavae sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nitumie fursa hii kuwaomba madiwani wote wa CCM wa Geita Mjini, Geita na wale wa Busanda ambao tulikuwa kwenye kikao kile jitokezeni muende wenyewe polisi, msikimbie nendeni wote polisi na terehe 9 na 10 tunaenda mahakamani na sare za CCM, na mimi kamanda wenu nawaambia kuwa tutashinda tumeweka mawakili tisa, milioni 12 dollar ni sawa na bilioni 29 halmashauri kama ya Geita peke yake huwa tunatumia bilioni 1.5 mpaka 1.8 maana yake wakitulipa hizo hela tunaweza kuwa na miaka 29 bila kumuomba Rais hela”alisisitiza Musukuma
Mbunge Musukuma wiki kadhaa zilizopita alikamatwa na jeshi la polisi na kulazwa ndani kwa masaa 24 kwa kile kilichoeleza kuwa alihusika kufanya vurugu kwenye mgodi wa Geita Gold Mine akiwa na madiwani mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanadaiwa walifunga barabara inayoingia
0 comments :
Post a Comment