Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza maafisa watatu wa TANESCO kuhakikisha umeme unarejea kote nchini hii leo la sivyo waandike barua ya kuacha kazi.
Dkt. Kalemani amesema hayo jijini Dar es salaam alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi One na ubungo na kutaka maelezo ya kukosekana kwa umeme nchini tangu jana na baadhi ya maeneo leo hii.
Maafisa waliopewa maelekezo hayo ni Mhandisi Isihaka Mosha-Meneja Udhibiti Mitambo, Mhandisi Bishaija Kahitwa-Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji na Abdalla Ikwasa-Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji.
0 comments :
Post a Comment