Taarifa
kutoka Butiama kwenye Mkoa wa Mara leo ni kuhusu miili ya watu wawili
kupatikana February 14 2017 kwenye Mgodi wa Buhemba ambapo kwa taarifa
za awali watu 13 wameokolewa wakiwa wamejeruhiwa baada ya kufukiwa ndani
ya mgodi.
Kutoka kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi amesema “Ni
kweli kabisa kwenye Wilaya ya Butiama Magunga ulipo mgodi wa zamani wa
dhahabu wa Buhemba shimo moja limefukiwa na kifusi saa 3 asubuhi”
“Mpaka
saa 7 mchana tuliweza kuokoa watu 13 na wengine wanaendelea na matibabu
huku wengine wakiwa wameruhusiwa wako nyumbani, kuna Wachimbaji wengine
wanne bado wanatafutwa na idadi inaweza kuongezeka”
“Idadi
inaweza kuongezeka kwasababu kuna Wachimbaji ambao huwa wanazamia bila
kujisajili majina yao kabla ya kuingia mgodini, wale ambao huwa
wanajisajili ndio rahisi kutambua rekodi zao… tunavyoendelea na zoezi”
– DC Annarose
0 comments :
Post a Comment