Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) wamekaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa muda usiozidi saa 24 baada ya kuwachapa Kagera Sugar mabao 2-1, na kuondoka na point 3 muhimu.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Obrey Chirwa dakika ya 40 ambaye aliitumia vyema krosi safi ya Ibrahim Ajib, huku bao la pili likifungwa na Ajib mwenyewe baada ya piga nikupige langoni mwa Kagera Sugar na mpira kumfikia Ajib aliyekuwa nje ya eneo la 18 na kuachia shuti kali la chinichini na kuandika bao la pili dakika ya 47.
Bao la Kagera Sugar limepatikana dakika ya 51 kupitia kwa Jafari Salum Kabaya aliyeunganishwa kwa kichwa mpira uliokuwa ukidakwa na kipa wa Yanga Youthe Rostand kutokana na kros ya Venance Ludovick.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba umeshuhudia Kagera Sugar wakionesha kandanda la ushindani ya kuonekana kuimudu Yanga, huku wakiongoza kwa umiliki wa mpira lakini wakishindwa kupata mabao ya kutosha kupata point yoyote.
Kwa vyovyote vile, Yanga itaondoka kileleni baada ya mechi ya kesho kati ya Simba na Mtibwa bila kujali aina ya matokeo yatakapatikana katika mchezo huo kwani endapo Mtibwa itashinda, itafikisha pointi 14 na kukaa juu ya Yanga, endapo Simba itashinda itakaa juu ya Yanga, na endapo Simba na Mtibwa watatoka sare, Simba itakalia usukani kwa tofauti ya