Kauli Ya Zitto Baada Ya Magufuli Kutohudhuria Sherehe Ya kuapishwa Kenyata



Zitto Kabwe amefunguka na kusema kitendo cha Makamu wa Rais Mhe. Samia kupokelewa na Balozi Kenya ni ishara kuwa mahusiano ya Tanzania na Kenya hayapo vizuri na kudai Rais Magufuli kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyatta inaweza kueleweka.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kitendo cha Rais Magufuli kutohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta inaweza kueleweka kwani kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.

"Makamu wetu wa Rais kupokelewa na Balozi ( sio hata Waziri wa Mashauri ya Kigeni au Waziri mwengine) ni dalili kuwa mahusiano yetu yanalega lega. Rais kutokwenda Kenya inaweza kueleweka maana hata Rwanda hakwenda kwenye uapishaji wa Paul Kagame" aliandika Zitto Kabwe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment