Meya Wa Ubungo Aachiwa Kwa Dhamana

Dar es Salaam. Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa polisi kwa takriban saa 15 akidaiwa kutaka kupanga njama za vurugu baada ya matokeo ya udiwani wa Kata ya Saranga kutangazwa.
Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chademaalikamatwa na polisi jana Jumapili Novemba 26,2017 saa tano asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Mtakatifu Peter, Kimara.
Akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu Novemba 27,2017 baada ya kuachiwa na polisi, Jacob amesema alipokamatwa alipelekwa vituo vya Mbezi kwa Yusuf, Mabatini na baadaye Oysterbay alikokaa muda mrefu.
"Nimeachiwa saa 7:40 usiku kwa dhamanahizi zote zilikuwa ni njama za kutunyima ushindi. Dhamana gani inatolewa usiku?” amehoji Jacob.
Amesema, "Hii ilikuwa mipango ili Chadema isishinde ila wakazi wa Ubungo wasivunjike moyo na haya, wamejionea hali halisi iliyofanyika na huu ni ushindi kwetu."
Jacob ambaye  pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay leo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment