Polisi Kenya Wausambaratisha Mkutano Wa Odinga

Mkutano wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance uliokuwa umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Jacaranda ili kuomboleza watu waliouawa na polisi hivi karibuni umesambaratishwa na polisi.

Polisi kuanzia mapema asubuhi walifunga eneo lote la Jacaranda ambako ingefanyika misa hiyo ya kumbukumbu sambamba na tukio la Rais Uhuru Kenyatta kuapishwa kuongoza muhula wa pili wa miaka mitano baada ya kushinda uchaguzi wa marudio Oktoba 26.

Mgombea urais kwa muungano wa Nasa, Raila Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo wa marudio akilalamikia kwamba hayakuwa yamefanyika marekebisho ya kutosha kuwezesha uchaguzi huo kuwa huru na haki.

Baada ya kususia Nasa wamekataa kutambua ushindi wa Uhuru na hawamtambui kama rais wa Kenya. Badala yake leo, wakati Uhuru akiapishwa, alipanga kuwaenzi wafuasi wake waliouawa katika makabiliano na polisi tangu ulipofutwa uchaguzi wa Agosti 8.

Polisi, ambao walikuwa wametangaza kwamba hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi mbali na wa sherehe za kuapishwa Uhuru, wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Nasa waliokuwa wanakusanyika nje ya uwanja huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment