YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI NA WAANDISHI WA HABARI DODOMA LEO
Nawashukuru wanahabari wote kwa kushiriki vyema katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru;
Napenda kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma.Idara imeshahamia Dodoma na huduma zote zinatolewa hapa;
Nawakumbusha press card zinamalizika muda wake Disemba 2017 hivyo wanahabari wanapaswa kuanzia Januari kuwahi kupata vitambulisho vipya kwa haraka kwani baada ya muda hakuna mwandishi ataruhusiwa kushiriki matukio makubwa bila press card.
Nizungumzie pia taarifa ya IMF ambayo wataalamu wake wamekamilisha kazi hapa nchini juzi kama ambavyo pia wamekamilisha tathmini kama hizo Afrika na kwingineko;
Ripoti yao ni nzuri na imebainisha mambo mazuri ambayo nchi imepiga hatua na changamoto ambazo tunaendelea kuzifanyiakazi;
Lakini kama kawaida kuna wanasiasa "vyuma vimekaza"-hawana ajenda bali kutafuta matukio na mwanya wa pa kusemea ili kuropokaropoka;
Sasa ngoja niwape mambo ya hakika kuhusu walichosema wataalamu hao. Ripoti yao imeonesha uchumi wa Tanzania upo imara, unakuwa kwa asilimia 6.8 kwa maana ya kuelekea nusu ya mwaka huu na mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 5 tofauti na nchi nyingine zilizofanyiwa tathmini.
Katika nchi ambazo zimefanyiwa tathimini kuanzia Novemba hadi Desemba mwaka huu Tanzania ipo juu kwa maana ya ukuaji kuna nchi moja ya Afrika wataalam hao wameeleza uchumi wake unakua kwa asiliamia 1.1 na huenda mwakani ukawa -1.
Taarifa ya IMF imeonesha nchi yetu imepata daraja ya juu kwamba imetekeleza vyema ushauri wa kitaalam iloyopewa maana mradi huu haukuwa wa fedha bali ushauri wa kitaalam;
Sisi kama nchi tumeridhishwa na maoni ya wataalam wa IMF na kwenye changamoto tutaendelea kuzifanyia kazi.
Niwapongeze wakulima kwani taarifa inaonesha mavuno mazuri ya mazao katika mwanzo wa mwaka huu yamesaidia sana upatikanaji wa chakula cha kutosha na hivyo kushusha bei za chakula.Tuendelee na kazi kubww mashambani na viwandani;
Taarifa za IFM zinaonesha mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 Novemba mwaka huu ikiwa ni chini ya lengo ambalo IFM ilidhani mfumuko ungekuwa asilimia 5 na zaidi.
Benki nyingi za Tanzania bado zina mitaji ya kutosha wameeleza wataalam hao na masuala ya changamoto za kushuka mikopo yanashughulikiwa lakini watanzania ni vyema wakajifunza kukopa na kulipa;
#Zoezi la kuhuisha takwimu za kiuchumi (Debasing) ni la kawaida chini ya mifumo ya upimaji uchumi duniani kwa lengo la kuongeza shughuli mpya za kiuchumi tofauti na anavyopotosha mwanasiasa mmoja ambaye ni dhahiri "vyuma vimekaza" hana tena ajenda anarukiarukia matukio na kuokoteza vitakwimu;
Zoezi hili la kuhuisha takwimu linaendelea katila nchi zote za EAC na Tanzaniq hii ni marq ya 5 kufanyika na matokeo yatatangazwa mwishoni mwa Disemba hii ili kuingiza mchango wa shughuli mpya za kiuchumi kama gesi, viwanda vipya n.k;
IMF wamesifu pia makusanyo yetu kutokana na utekelezaji wa sera.Ndio maana makusanyo ya Serikali yameongezeka kutoka tril. 9.9 mwaka 2015 hadi Tril 14 mwaka 2017 kwa wastani wa mwaka;
Wametusifu pia kuwa Serikali yetu inajitahidi kulipa madeni na kama mlivyosikia juzi Rais amesema katika miaka miwili hii ameshalipa madeni ya zaidi ya TZS bilioni 900 na nyingine uhakiki unaendelea na atalipa fedha hizo zipo hakuna shida;
Tufike hatua kama watanzania katika kujenga nchi yetu kwenye kufikia Tanzania tunayoitaka, tujue sio kila kitu ni siasa kuna mambo ni uchumi wa nchi na kuna mambo ni maendeleo hayapaswi kufanyiwa tashtiti;
Katika tathmini hizi ambazo pia zimefanyika nchi mbalimbali ipo nchi moja kubwa tu ya Ulaya imeelezwa kuwa na changamoto nyingi za kiuchumi katika tathmini ya uoande wa nchi zilizokopeshwa fedha.
Sisi tupo vizuri na tunafanyiakazi changamoto zilizoainishwa kama vile mikopo chechefu na kuendelea kukusanya kodi na kuboresha sekta binafsi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*
0 comments :
Post a Comment