Zanzibar heroes imeungana na Kenya kucheza fainali Jumapili baada ya kuichapa Uganda mabao 2 kwa 1 katika patashika ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa.
Zanzibar heroes ndo ilikuwa timu ya kwanza kuandisha bao lililofungwa na Abdul - Azizi Makame baada ya Ibrahim Ahmada kuwakosakosa na kusababisha kona.
Uganda walisawazisha bao hilo dakika 6 baada ya Zanzibar kutangulia, mabao yaliyodumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Mohamed Issa Banka dakika ya 58 aliiandikia Zanzibar bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Ahmada kuangushwa ndani ya 18 na Nsubugu Joseph ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Hadi kufikia dakika 90 za mtanange huo Zanzibar heroes 2 na Uganda 1.
0 comments :
Post a Comment