Ajali Mwanza Watano Wafariki




TAREHE 16.12.2017 MAJIRA YA SAA 19:30HRS USIKU KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA ENEO LA MTAA WA BUHONGWA NA KATA YA BUHONGWA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.107 BKK TOYOTA COASTER MALI YA KAMPUNI YA AUKI WA MWANZA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BADRU HABIBU, MIAKA 33, MKAZI WA NYEGEZI – MWANZA, LIKITOKEA KATORO GEITA KUJA MWANZA LILIGONGANA NA GARI LENYE NAMBA T.504 BZB SCANIA LORRY LENYE TELLA LENYE NAMBA T.880 ASA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SALIM OMARY, MIAKA 28, MKAZI WA DAR ES SALAAM, LIKITOEA MWANZA KWENDA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUSABABISHA VIFO KWA WATU WA TANO NA MAJERUHI KUMI NA  TATU WOTE ABIRIA WALIOKUWEPO KWENYE GARI LA AINA YA TOYOTA COASTER.

MAREHEMU WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO HADI SASA AMETAMBULIKA JINA MMOJA TU AMBAYE NI 1. ABDUL MUSTAFA, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 42 HADI 45, HUKU MAREHEMU WENGINE WA NNE MAJINA YAO BADO HAYAJAFAHAMIKA. AIDHA MAJERUHI WOTE KUMI NA TATU WAPO HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAKIPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MIILI YA MAREHEMU PIA IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA GARI LA TOYOTA COASTER ALIYEJARIBU KUYAPITA MAGARI MENGINE YA MBELE BILA KUCHUKUA TAHADHARI KISHA KUSABABISHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO NA MAJERUHI KWA WATU. MADEREVA WOTE WA MAGARI HAYO WAMEKAMATWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WAHUSIKA/MHUSIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA AKIWATAKA KUWA MAKINI PINDI WAWAPO BARABARANI HUKU WAKIJUA WAMEBEBA ROHO ZA WATU, HIVYO WAZINGATIE SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO NA MAJERUHI VYA AINA KAMA HII VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA PIA AMEWAOMBA ABIRIA KUTOA TAARIFA POLISI MAPEMA KWA MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUEPUSHA VIFO KWA WATU WASIO NA HATIA. PIA ANAWAOMBA WANANCHI KWENDA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KUTAMBUA NDUGU ZAO AMBAO WENGINE NI MAJERUHI LAKINI WENGINE WAMEPOTEZA MAISHA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment