SAKATA la kugombea maiti lililoleta sintofahamu ya nani mwenye haki ya kuzika mwili wa marehemu,MARY BATHOLOMEW lililodumu mjini Manyoni kwa takribani siku mbili, limepatiwa ufumbuzi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida kutoa maamuzi ya upande wenye haki ya kuuzika mwili huo.
MSUGUANO wa sakata hilo kwa mujibu wa maelezo yaliyowasilishwa Mahakamani hapo,umetokana na kuwepo kwa dini tofauti kati ya familia hizo mbili,ambapo kwa upande wa mke alikuwa ni muumini wa dini ya kikristo na kwa upande wa mumewe alikuwa muumini wa dini ya kiislamu.
HATA hivyo baada ya kusikilizwa kwa msuguano huo wa pande zote mbili,yaani waweka pingamizi na wajibu maombi ya pingamizi hilo,ndipo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Manyoni ikafikia maamuzi
AKITOA maamuzi ya kesi hiyo ya madai namba 1 ya mwaka 2018,Hakimu Mfawidhi Mkazi wa Mahakama ya wilaya hiyo, BWANA FERDINAND KIWONDE amesema kwa mujibu wa sheria na kupitia vifungu vya sheria ya ndoa na katiba ni kwamba ridhaa ya wazazi itatakiwa endapo tu wanaooana hawajafikia umri wa miaka 18.
AIDHA Hakimu huyo amefafanua kwamba uthibitisho wa dini kwa mujibu wa sheria ni mfumo aliokuwa akiishi nao marehemu ndani ya ndoa yake iliyofungwa kiislamu kama uthibitisho wa cheti cha ndoa ulivyoonyesha na kwamba ameiishi kwa misingi ya kuamini dini ya kiislamu pasipo ubishi wowote.
AMESEMA kifungu cha 41 cha sheria ya ndoa miongoni mwa mambo yasiyobadilisha ndoa ni pamoja na mahari,hivyo kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamni hapo,ndipo Mahakama ikatoa tamko la kwamba mwili huo unastahili kuzikwa kwa kuzingatia sheria,taratibu na misingi yote ya dini ya kiislamu,huku upande wa pili ukikaribishwa kushiriki zoezi hilo la mazishi kwa uhuru zaidi.
0 comments :
Post a Comment