Unaweza kusema kuwa imani, morali na maneno ya kutia moyo kutoka kwa kocha Aristica Cioaba kwenda kwa wachezaji wa Azam FC, ndiyo iliyokuwa siri kubwa kwa timu hiyo kuinyuka Simba katika mchezo wa jana wa kundi A kuwania Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Azam imekutana na Simba ikiwa imetoka kupoteza mchezo wake dhidi ya URA kwa kufungwa bao 1-0, na ilikuwa inahitaji ushindi wa lazima katika mchezo dhidi ya Simba licha ya wachezaji kuingia kwenye mchezo huo wakiwa wamekata tamaa. “Uliona baada ya mchezo dhidi ya URA wachezaji walihuzunika kwa matokeo na wengine walilia jambo kubwa lilikuwa huenda tungepoteza na tusiingie nusu fainali, nikaongea na wachezaji na kuwapa morali nikawaambia bado nawaamini mimi pamoja na uongozi,” amesema kocha huyo raia wa Romania na kuwashukuru wachezaji kwa namna walivyopambana kwenye mchezo huo na kupata ushindi.
Kwa mujibu wa kocha huyo baadhi ya maneno ambayo aliwaambia wachezaji wake kabla ya mchezo dhidi ya Simba ni haya:- “Leo (jana) inatakiwa kupambana ili kila mmoja aone kuwa Azam haijafanya 'sapraizi' bali ipo nafasi ya kwanza kama Simba, kila mmoja anatakiwa kuingia uwanjani leo na kupambana na watu kuona kuwa Azam ina wachezaji wazuri na timu nzuri na inatakiwa kushinda mchezo,” alisema.
Cioaba amesema kuwa wachezaji waliiingia uwanjani na kuheshimu mbinu alizowapa na kila kitu na kudai kuwa anafuraha kubwa na aina ya kikosi alichonacho. “Ndani ya siku saba nilikuwa na mechi tano, baadhi ya wachezaji wamecheza dakika 90 kwenye mechi tatu na walikuwa wamechoka lakini kila mmoja alikuja kwangu na kuniambia kuwa kocha nahitaji kucheza mchezo huu na kupambana katika mchezo huo na kushinda
0 comments :
Post a Comment