Mwenyekiti Wa Bodi ya Parole,ambaye pia ni mwenyekiti Wa kudumu Wa chama cha siasa chaTLP Dr.Agustino Mrema amesikitishwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia katika hospital ya rufaa ya KCMC kutokana maradhi ya kisukari.
Amesema kuwa taarifa hizo zinaenezwa na wapinzani wake wakiitamani nafasi ya umwenyekiti Wa parole aliyopewa na rais Magufuli.
Ameongeza kuwa watu hao hawajaanza leo uzushi kwani pia waliwahi kumzushia kuwa ni mgonjwa asichaguliwe wakati akigombea ubunge jimbo LA vunjo na kusababisha kuukosa ubunge wake.
"Hawa wapinzani wangu wameingiwa kiwewe wamesikia naenda vunjo kutoa shukrani kanisani wameanza kuhaha na kusambaza uzushi Wa kifo kwenye mitandao ya kijamii.Mrema nipo sinza bado nadunda nitakufa lakini si wanavyotaka wao"
Ameongeza kuwa taarifa za kuzushiwa kifo si Mara ya kwanza kuzisikia kwani wapinzani wake wanamwonea donge kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa parole na sasa afya yake imeimarika .

0 comments :
Post a Comment