Siku mbili baada ya kukamatwa na polisi kwa mahojiano kwa Tito Machibya, maarufu Nabii Tito, anadaiwa kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe tumboni na kushonwa nyuzi 25.
Nabii Tito alikamatwa na polisi mkoani Dodoma kwa kosa la kufundisha mafundisho yaliyo kinyume na dini kwa kuhamasisha watu kunywa pombe kwani si dhambi na kuoa wafanyakazi wao wa ndani ambapo hata hivyo, jeshi hilo lilisema nabii huyo ana matatizo na akili yaliyothibitishwa na daktari kati aHospitali ya vicha ya Milembe mkoani Dodoma.
Inadaiwa kuwa, leo polisi waliambatana na nabii huyo nyumbani kwake Ng’ong’ona mkoani humo kwa ajili ya upekuzi ambapo aliingia ndani na kutoka akiwa anavuja damu tumboni huku ameshikilia wembe mkononi ambapo iliwalazimu polisi hao kumkimbiza Zahanati ya Polisi ya Mkoa wa Dodoma.
Mmoja wa madaktari wa zahanati hiyo kwa sharti la kutotajwa jina amesema nabii huyo alifikishwa, saa tisa alasiri akiwa na jeraha kubwa tumboni.
“Alifikishwa na kushonwa nyuzi 25 na kuruhusiwa kwani hakuwa na shida nyingine yoyote halafu jeraha lake halikufunguka kwa ndani sana, kwa hiyo hakutoka damu nyingi sana alitibiwa na kuondoka na askari.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto alipoulizwa kuhusu tukio hilo hilo alisema hana taarifa.
0 comments :
Post a Comment