Aliemuapisha Odinga Aachiwa Huru Kwa Dhamana


Mbunge wa eneo bunge la Ruaraka nchini Kenya aliyehusishwa na kiapo cha kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ameachiliwa kwa dhamana ya ksh.50,000 baada ya kulala katika seli za kituo cha polisi.
Tom Kajwang alifikishwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi Alhamisi jioni ambapo alitarajiwa kukabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kushiriki katika mkutano na kula kiapo kinyume na sheria.
Wabunge wa Nasa waliojaa katika mahakama hiyo walisema kuwa mashtaka aliyowekewa Kajwang ni bandia.
Kajwang alilala katika kituo cha polisi cha Kiambu baada ya kukamatwa siku ya Jumatano kwa kile maafisa wanasema ni jukumu lake katika sherehe ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa 'rais wa wananchi'.
Mbunge huyo ambaye alisimama nyuma ya Raila wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika uwanja wa Uhuru Park Jijini Nairobi alikamatwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi na kupelekwa makao makuu ya ujasusi ili kuhojiwa.
Kesi yake itaendelea tarehe 6 wiki Ijayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment