Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhamis ) akiwa nyumbani kwake.
Taarifa hiyo imethibitishwa na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu alipowasili katika kipindi cha 'East Africa Breakfast' kinachorushwa kutoka East Afrika Radio.
"Ni kweli Tambwe Hizza amefariki nami nimetumiwa ujumbe mfupi mara nilipofika hapa East Afrika Radio kama kiongozi wa chama, hivyo naomba tupewe muda kidogo ili tuweze kufahamu zaidi chanzo cha kifo chake maana imekuwa ghafla sana kutokana mpaka jana usiku saa 5 nilikuwa nae", amesema Mwalimu.
Kwa upande mwingine, Salum Mwalimu amesema mpaka jana marehemu Tambwe Hizza alikuwa nae katika kuomba ridhaa kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ili aweze kuwa Mbunge wa Jimbo hilo katika siku za usoni.
0 comments :
Post a Comment