Balozi wa Uturuki nchini Mh. Ali Davotuglu amewakabidhi tuzo na medali, wachezaji ambao wamepata mafanikio katika mechi mbalimbali za timu hiyo ikiwemo tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba.
Hafla hiyo ambayo imefanyika jana usiku nyumbani kwa balozi huyo golikipa namba moja nchini Aishi Manula alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba wa klabu ya Simba.
Mbali na tuzo hiyo ya Manula wachezaji wengine walikabidhiwa medali za kuwa wachezaji bora wa mechi nne zilizopita ambao ni nahodha John Boko ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Ndanda FC.
Mwingine ni kiungo Said Ndemla ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar iliyopigwa mkoani Kagera na Ndemla kufunga bao moja pamoja na kusaidia jingine moja kwenye ushindi wa mabao 2-0.
Hafla hiyo maalumu iliandaliwa na Ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya kujenga na kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya klabu ya Simba na nchi ya Uturuki.
0 comments :
Post a Comment