Basi la abiria mali ya kampuni ya Tahmeed coach linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda nchini Kenya jijini Mombasa limepinduka leo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi watu wengine zaidi ya 20.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa basi hilo limepinduka katikati ya Msata na Kabuku mkoani katika eneo la Kitumbi Tanga na kudai kuwa mtu mmoja alifariki hapo hapo huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa.
"Ni kweli ajali imetokea imesababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 20, majeruhi wengine walipata majeraha madogo madogo hivyo tayari wamesharuhusiwa lakini majeruhi wengine watano nado wanapata matibabu"
Hii ni ajali ya pili kwa mwaka huu inayohusisha basi za Tahmeed kutokea katika eneo la Kitumbi, Januari 29, 2018 basi jingine liliwaka na kuteketea kwa moto katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.
0 comments :
Post a Comment