Mwalimu wa shule ya msingi Dutumi iliyopo tarafa ya Mvuha Morogoro aliyefahamika kwa jina ya Rahaleo Salehe Kazimbaya amejinyonga hadi kufa kwa kutumia Kanga kujitundika kwenye mti wa Mwembe mda mfupi baada ya kumuua mkewe Sikilinda Magumba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la polisi bwana Rahaleo Kazimbaya usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake mtaa wa Kambi Tano, Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro alimuuwa mkewe huyo kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali kwenye mwili wake na kupelekea kupoteza maisha, kisha baada ya kutukeleza mauaji hayo na yeye alichukua kanga na kujinyonga.
Mpaka sasa bado haijafahamika nini chanzo cha mwalimu huyo kufanya muaji hayo kwa mkewe kisha na yeye kujinyonga, ila jeshi la polisi limechukua miili ya watu hao mtu na mkewe na kwenda kuihifadhi mochwari.
Aidha Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kufuatia vifo hivyo .
0 comments :
Post a Comment