Kubenea Awaonya Ccm

Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea amevitaka vikundi vinavyodaiwa kuwa vya CCM vinavyozunguka kuandikisha vitambulisho vya watu kuacha mara moja kabla hawajachukua hatua ambazo amezitaka zisilaumiwe.
Akizungumza jana na wanahabariKubenea alisema kwamba wamegundua wapo vijana ambao wamekuwa wakilizunguka jimbo la Kinondoni na kuwalaghai wapiga kura kwa kununua vitambulishokuchukua shahada pamoja na kununua vitambulisho hivyo ili kupunguza idadi za wapiga kura kwa makusudi.
Kubenea amesema kwamba endapo vikundi hivyo vitakaidi agizo hilo watashughulikiwa kama wahalifu kwani kitend wanachokifanya ni kitendo cha uhalifu.
"Mnyika alituambia  kuwa wanaofanya hivyo ni vibaka kama vibaka wenginehivyo wanapaswa kushughulikiwa.  Na sisi tunasema kwamba Tutaingiza vijana wetu mitaani ili washughulikiwe na lolote litakalotokea wasituulize." Kubenea
Pamoja na hayo kubenea amesema kwamba tayari wamekwishapeleka malalamiko yao katika vyombo husika.
Kubenea kwa sasa ndiye Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Salum Mwalimu wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Februari 17
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment