Leo March 28, 2018 Mazishi ya Allen Achiles Mapunda (20) aliyefariki March 25, 2018 katika hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya na kifo chake kuzua utata yamefanyika katika makaburi ya Iyela jijini Mbeya na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali jiji la Mbeya.
Mwili wa marehemu umepokelewa kutoka hospitali ya Rufaa majira ya saa kumi eneo la Mafiat na kushushwa kwenye gari na kubebwa begani hadi nyumbani kwao huku vijana wakiimba nyimbo za maombolezo.
Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji Andrew Kalata wa Kanisa la EAGT Kisima cha Bubujiko lililopo mtaa wa Iyela II amesema maisha ya mwanadamu yanaweza kutoweka muda wowote lakini unapokufa uwe na ushuhuda mzuri kama ulivyo kwa Allen,
“Allen alikuwa ni Shemasi wa Kanisa na mwalimu wa uimbaji na mtoaji mzuri wa sadaka nami nilikula matunda ya biashara yake machungwa “ -Mchungaji Kalata.
0 comments :
Post a Comment