Mwanamke mmoja kutoka nchini Ufaransa amedai kuwa anakabiliana na faini ya Dola za Marekani 500 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 1.2 baada ya apple alilokuwa amepewa bure kwenye ndege kukutwa kwenye begi lake.
Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Crystal Tadlockambaye alikuwa anasafiri kutoka Paris, Ufaransa kwenda Marekanialipewa apple hilo kama kitafunwa kwenye ndege aliyokuwa amepanda.
Anaeleza kuwa aliamua kulitunza ili kulila akiwa amepanda ndege yake inayofuata akiwa anaelekea Denver lakini lilikutwa wakati wa ukaguzi na mawakala wa mipaka wa Marekani aliposhuka kwenye ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Minneapolis.
0 comments :
Post a Comment