Waziri Mkuu wa Armenia, Serzh Sargsyan amejiuzulu rasmi leo April 23, 2018 baada ya siku kadhaa za maandamano makubwa ya kitaifa dhidi yake.
Wafuasi wa upinzani wanamtuhumu Sargsyan kwa kung’ang’ania madaraka mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu Jumanne ya wiki iliyopita, baada ya kumaliza mihula miwili ya miaka 10 kama Rais
Tangazo hilo limekuja baada ya kiongozi wa upinzani Nikol Pashinyan kufunguliwa kutoka kizuizini. Pashinyan alikamatwa siku ya Jumapilibaada ya mazungumzo ya televisheni na Mr Sargsyan kutofikia muafaka.
0 comments :
Post a Comment