Kichuya awatoa hofu wana Simba


NYOTA wa Simba na kipenzi chama mashabiki wa timu hiyo, Shiza Kichuya, amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa klabu hiyo juu ya mustakabali wake ndani ya timu hiyo.

Kichuya ambaye alikuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu, inaelezwa mkataba wake unamalizika mwezi huu na ametajwa kuwindwa na klabu za Yanga na Azam. 

Akizungumza jana muda mfupi kabla timu hiyo haijaenda Kenya, Kichuya, alisema suala la usajili litajulikana akirejea kutoka kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu. 

"Suala la usajili litajulikana tu, kwa sasa akili yangu na hata wachezaji wenzangu tunaielekeza Nairobi kwenye michuano ya Sportpesa lengo tunataka ubingwa," alisema Kichuya. 

Aidha, alisema suala la usajili ni la makubaliano na pindi kila kitu kikikamilika usajili wake utakuwa wazi ni timu gani atajiunga nayo lakini anaipa nafasi kubwa klabu yake ya Simba.

Kichuya, ametoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba na kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuukosa kwa zaidi ya miaka minne. 

Nyota huyo alijiunga na Simba msimu wa mwaka 2015/2016 akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kiungo huyo yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu iliyotangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment