Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kueleza kuwa hakuna mchezaji yoyote anayejuta kuwachezea mabingwa mara 27 wa ligi kuu bara.
Mkwasa amesema kuwa Yanga ni sehemu nzuri ya kuwa na wachezaji hivyo hakuna yeyote atakayeweza kujuta endapo atajiunga na kikosi cha timu yao ingawa akisema ni msimu huu tu pekee mambo yajakaa vizuri.
Katibu huyo ameeleza Yanga haijawaka na msimu mzuri kipindi hiki kutokana na kuyumba kifedha lakini anaamini kuwa klabuni kwao bado ni sehemu ambayo mchezaji anaweza akaonesha kile alichonacho.
Kauli hiyo ya Mkwasa imekuja kufuatia tetesi mbalimbali zilizoeleza kuwa itaondokewa na wachezaji wao kuelekea sehemu zingine ambazo amezikanusha kuwa hazina ukweli.
"Hakuna mchezaji anayejutaka kuichezea Yanga kwa maana ni sehemu salama ya wachezaji" amesema Mkwasa.
Mapema jana baada ya kukutana na Kelvin Yondani, Mkwasa aliyaeleza hayo na kusema kuwa hakuna ukweli wa taarifa hizo na akiomba zipuuzwe ikiwemo ya Yondani aliyehusishwa kwenda Simba pamoja na Azam FC
0 comments :
Post a Comment