Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi
(kushoto) akizungumza na Mjumbe mwenzake, Prof Costa Mahalu katika
Viwanja vya Bunge hilo, mjini Dodoma jana. Picha na Michael Jamson
Na Musa Juma na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Posted Jumatano,Marchi19 2014 saa 8:57 AM
Posted Jumatano,Marchi19 2014 saa 8:57 AM
Kwa ufupi
- Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge hilo tayari kwa kuijadili, kuiboresha na hatimaye kutoka na Rasimu ya Tatu itakayopigiwa kura ya ama kuikubali kuwa Katiba Mpya au la.
Dodoma/Dar: Baadhi ya wasomi na
wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini wamesema hotuba ya
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
itasaidia kubadilisha msimamo wa wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Jaji
Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge hilo tayari
kwa kuijadili, kuiboresha na hatimaye kutoka na Rasimu ya Tatu
itakayopigiwa kura ya ama kuikubali kuwa Katiba Mpya au la.
Mwanasiasa mkongwe, Njelu Kasaka alisema hotuba
hiyo imesaidia kutoa uelewa wa mambo kwa kuwa idadi kubwa ya wajumbe
ndani ya Bunge hilo hawakuwa na uelewa juu ya hoja mbalimbali
zilizopendekezwa kwenye rasimu hiyo.
“Kutokana na ufafanuzi huo, wengi watakuwa
wameelewa kwa nini Tume iliamua kupendekeza muundo wa Serikali Tatu na
wala siyo mbili. Itasaidia pia kuwajengea uwezo wa kuhoji katika
mijadala ya Kamati itakapoanza kukaa rasmi,” alisema Kasaka ambaye
alikuwa miongoni mwa Wabunge 55 walioasisi Kundi la G55 lililotaka
kuundwa Serikali ya Tanganyika mwaka 1993.
“Lakini jambo jingine hotuba hii imeondoa ni
unafiki na imewaaibisha kwa unafiki wao baadhi ya watu, kwa sababu
pamoja na kuongoza Serikali moja ya Jamhuri ya Muungano, imefahamika
wazi kwamba Waziri Mkuu kumbe hana mamlaka yoyote yale katika upande wa
Zanzibar.”
Kwa upande wake, Profesa Boniventure Rutinwa wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aliunga mkono hoja hiyo akisema
kinachotakiwa kwa wajumbe hao ni kujenga imani, kuondoa tofauti zao na
kutokubaliana na hoja zenye masilahi ya vyama na makundi yao badala ya
Taifa.
“Kinachotakiwa kwa sasa ni kupima uwezekano kwa
kuhoji, je, pamoja na ufafanuzi huo, Serikali Tatu inaweza kuwa
mwarobaini wa kumaliza changamoto zote? Lakini pia wanatakiwa kufahamu
kwamba inawezekana kuna changamoto nyingine ambazo zinaweza kujitokeza
katika muundo huo,” alisema Profesa Rutinwa.
Kwa upande wake, Profesa Penina Mlama aliwataka
wajumbe wa Bunge hilo kuchukua hoja hizo na kufikiri kwa mapana zaidi
wakati wa majadiliano ili kuondoa athari zinazoweza kujitokeza baadaye.
“Wamerahisishiwa, na kazi imebakia kwao kupima na
kufikiria zaidi hotuba hii. Wajumbe watambue kwamba si mawazo ya Jaji
Warioba yaliyowasilishwa pale, bali ni mawazo ya Watanzania, ambayo
yanatakiwa kupokewa kwa mtazamo chanya ili wasije kuaibika baadaye iwapo
watashindwa kufanya uamuzi sahihi,” alisema.
Mjumbe wa Bunge, James Mapalala alisema Jaji
Warioba amemaliza kazi ya kuelimisha juu ya umuhimu wa Serikali Tatu
na anaamini watakaosimama kumpinga wataona haya.
- Sitta yu msalabani, kuongoza Bunge Maalumu la Katiba?
- Ujumbe wa Kwaresima 2014 na wanasiasa wetu nchini
- TRA Mbeya yakiri wingi wa kodi nchini
- Exim: Wekeni fedha benki
- Jazba iepukwe katika kujadili Rasimu ya Katiba
- Mjue Torongey chaguo la Chadema Chalinze
- CCM kuzindua kampeni Chalinze leo
- Miradi kukabili foleni yasuasua
- Wanafunzi wamkata panga mwalimu wao
- Ardhi, uraia vyazua dukuduku
- Bunge lachafuka mjini Dodoma
- Tundu Lissu: Sitta ananitonesha vidonda
- Jaji Warioba ateka Bunge
- Ukawa waeleza sababu za ‘kumzuia’ Warioba
- Maajabu ya Shule ya Sekondari Tongoni
- Shibuda amwangukia JK kuhusu Muungano
- #Katiba Bungeni: Warioba aibua mjadala wa serikali tatu [VIDEO]
- Warioba awakuna wasomi
- ‘Sina njaa, sigombei tena’
- Mgimwa asubiri baraka za JK Bunge la Katiba
- Mbunge wa Chadema alia
0 comments :
Post a Comment