Thursday, June 25, 2015
Nkupamah blog
Mwanamitindo na Msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo, maarufu kama ‘Kidoti’ amejikuta akiambulia matusi ya nguoni kwa kosa la kumpongeza msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Ali Kiba baada ya kutwaa tuzo tano za Kili Music Awards zilizotolewa mwezi huu jijini Dar.
Mwanadada
huyo ameioga mvua hiyo ya matusi katika akaunti yake ya Mtandao wa
Kijamii wa Intagram kwa watu tofauti kwa kile kilichodaiwa kuwa anahaha
baada kuachwa na Mbongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ ambapo ameamua
kufanya hivyo ili kuupoza mtima wake na kwa sasa kuna taarifa kwamba Ali
Kiba ndiye anayemmiliki mtoto huyo.
Baada ya kutokea ishu hiyo, Mwandishi alimtafuta Jokate ili kusikia anazungumziaje hilo ambapo alisema: “Nashindwa
kuielewa jamii inataka mtu aishi vipi, lakini yote kwa yote siwezi
nikamkandia mtu kwenye muziki wake, kwa upande wangu mimi ni shabiki wa
Ali Kiba kwa sababu ninapenda kazi zake na hakuna wa kunizuia kufanya
chochote juu yake.”
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment