Friday, June 26, 2015
Nkupamah blog
Mrembo anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
Ndani
ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, mwandishi
wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake
jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini
hapo.
Mbali
na kunaswa siku hiyo, pia mwandishi wetu amekuwa akiwashuhudia mara
kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe
jijini Dar.
Mara
ya mwisho, Linah na Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji
wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar, mapema mwezi huu.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment