Friday, June 26, 2015
Nkupamah blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Waziri aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Profesa Sospeter Muhongo, jana aliumbuka baada ya Chama chake kukataa kupokea lundo la makasha ya CD (santuri) zenye picha za wadhamini wake 675.
Badala yake, alielezwa kwamba, hakuna kipengele kinachoruhusu kuwa na kumbukumbu hiyo.
Profesa
Muhongo, alirejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa na chama hicho
kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, saa 9:57 asubuhi na
kumkabidhi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na
Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatibu kwenye makao makuu ya chama hicho
mjini Dodoma.
Baada
ya kukabidhi fomu za wadhamini wake katika mikoa 15 aliyopita, Profesa
Muhongo alitoa pia makasha 15 yenye CD za picha ambazo alidai amefanya
hivyo ili kuonyesha hajapita njia ya mkato akidai anaamini mtu sahihi
atakayeweza kuwavusha watanzania kwa sasa, ni yeye na si mgombea
mwingine kati ya makada wote waliojitokeza kutaka kumrithi Rais Jakaya
Kikwete.
Alipomaliza kuzungumza na kisha kukabidhi CD hizo, Khatibu alisema:”Bahati
mbaya katika Daftari la kurejesha fomu za CCM za kugombea kiti cha
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 2015 hakuna mahala
panapoonyesha kwamba utapaswa kukabidhi CD ulizonipa…wanaangua
(vicheko).”
Baada ya kuelezwa hivyo, aliondoka na kuziacha CD hizo kwa Khatibu.
Profesa
Muhongo alijiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini, baada ya kuhusishwa na
kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya
Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na baadaye kutangaza
nia ya kugombea urais.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment