Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa
(kulia) pamoja na Rais wa Cambridge Development Initiative (CDI), Bw. Ravi Solanki wakitia saini
makubaliano ya kuimarisha elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini jana jijini
Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Afisa Mwandamizi wa uwekezaji, NEEC, Bw. Oswald Karadisi
(kulia) na Mkurugenzi Ujasiriamali wa CDI, Bi. Georgia Ware.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa
(kulia) akipongezana na Rais wa Cambridge Development Initiative (CDI), Bw. Ravi Solanki
(kushoto) baada ya kutia saini makubaliano ya kuimarisha elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi
wa vyuo vikuu nchini jana jijini Dar es Salaam. katikati ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali wa CDI, Bi.
Georgia Ware.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limefikia makubaliano
na Cambridge Development Initiative (CDI) ili kuimarisha mafunzo ya
maswala ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.
CDI ni
mpango ulioasisiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini
uingereza ambapo wanafunzi wenye vipaji toka chuo hicho na vyuo vikuu
hapa nchini wanakutana, kubadilishana uzoefu ili kutatua changamoto
mbalimbali.
Mkataba
wa makubaliano hayo umetiwa saini na Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi.
Beng’i Issa wakati Rais wa mpango huo, Bw. Ravi Solanki aliwakilisha
wenzake.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kutia saini
mkataba huo, Bi. Beng’i alisema elimu na maarifa ya ujasiriamali ni
muhimu sana kwa sasa ambapo changamoto ya ajira ni kubwa dunia nzima,
Tanzania ikiwa mojawapo.
“Mzingatie sana maarifa mnayopata hapa…yatawasaidia katika maisha yenu,” aliwaasa wanafunzi hao.
Kwa
sasa jumla ya wanafunzi 36 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini
wanaendelea na mpango huo wa ujasiriamali yanayoitwa DAREnterprisers kwa
muda wa miezi miwili yanayofanyika katika kituo cha Ujasiriamali cha
chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Ujasiriamali wa mkakati huo, Bi. Georgia Ware alisema ni imani ya
mradi huo kuwa wanafunzi wanaweza kubadilisha dunia na kuwa sehemu bora
ya kuishi.
“Wote hawa wana ujuzi na vipaji vyao, na kwa umri wao mdogo bado wana uwezo wa kujifunza mambo mengi,” alisema.
Alisema
kama kila mmoja wa wanafunzi hao wanaopata mafunzo hayo akimshawishi
mwenzake kufanya ujasiriamali basi jiji la Dar es Salaam linaweza
kubadilika kwa kiwango kikubwa katika miaka mitano ijayo.
Katika
mafunzo yanayoendelea, wanafunzi hao wanafundishwa kuhusu umeme
mbadala, usafi wa maji na taka ngumu na jinsi ya kutunza miji.
Rais
wa mpango huo, Solanki amesema mbali ya kuwapatia maarifa wanafunzi hao
yatakayowawezesha kuwa wajasiriamali, pia program hiyo inalenga
kuwafanya vijana kutatua changamoto katika jamii zao.
Mmoja
wa wanaofaidika na mafunzo hayo, Katera Ahad amesema wanatarajia kupata
maarifa yatakayowawezesha kujinoa katika mambo wanayotaka kutekeleza
kama wajasiriamali.
Mpango huo ulianza mwaka 2013 ambapo wanafunzi 20 hapa nchini walifaidika na wanaendelea na miradi yao mbalimbali.
Hivi
karibuni NEEC ilizindua mwongozo wa Taifa wa Ufundishaji Ujasirimali
(NETF) katika shule na vyuo ili kuwawezesha vijana wa kitanzania na
wananchi kwa ujumla kuwa na elimu hiyo na kuchochea maendeleo.
Poste by Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment