Published in Nkupamahmedia
Real
Madrid leo wameichapa 4-1 Manchester City nchini Australia katika mechi
ya maandalizi ya msimu na kumaliza vinara kwenye msimamo wa mashindano
ya International Champions Cup, yaliyojumuisha pia
klabu ya AS
Roma.Baada ya mechi hiyo, Real Madrid walipata kombe ambapo Alvaro
Arbelo na Cristiano Ronaldo walinyanyua ndoo hiyo.
Cha kushangaza, Sergio Ramos hakuwepo kwenye tukio hilo wakati yeye ndiye nahodha wa timu baada ya Iker Casillas kuondoka.
Ramos alitolewa na akamkabidhi kitambaa cha unahodha, Arbeloa, lakini bado Ronaldo alirudi kubeba kombe.
Ramos alikuwa wapi?
Hata kama ni kombe la Pre-season, ilifikirika kwamba ingekuwa bahati kwa Ramos kubeba kombe kwa mara ya kwanza akiwa nahodha.
Au alikuwa na majukumu mengine?
Kama kweli Ramos anataka kujiunga na Manchester United, majira haya ya kiangazi huenda hakutaka kunyanyua kombe hilo.(P.T
0 comments :
Post a Comment