Kampuni
ya Coca-Cola Afrika ya Kati, Mashariki na Magharibi imezindua kampeni
mahsusi ijulikanayo kama ‘Sababu Bilioni za Kuamini’ inayolenga
kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kujiamini pindi wanapopita katika
changamoto mbalimbali zinazowakabili kimaisha kabla ya kutimiza ndoto
zao. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itaendeshwa nchi nzima.
Nyota
wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ni miongoni mwa vijana
wanaotolewa mfano katika dhana hii. Alitengeneza single zaidi ya 20
kabla ya kufanikiwa na hatimaye kufikia katika mafanikio makubwa
aliyonayo sasa.
Diamond kabla ya mafanikio.
Diamond kabla ya mafanikio.
Mwaka
2007 Diamond alifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuza
mitumba, kufanya kazi katika vituo vya kujaza mafuta pamoja na kupiga
picha mitaani ili aweze kupata fedha zilizohitajika studio.
Diamond Platnumz
Hata hivyo, hakukata tamaa na ni kutokana na moyo wake huo wa kutokubali kushindwa kwa urahisi ameweza kufanikiwa na kuwa miongoni mwa nyota wachache wa muziki anayetamba aliye kijana tajiri mkubwa kwa sasa hapa nchini.
Diamond Platnumz
Hata hivyo, hakukata tamaa na ni kutokana na moyo wake huo wa kutokubali kushindwa kwa urahisi ameweza kufanikiwa na kuwa miongoni mwa nyota wachache wa muziki anayetamba aliye kijana tajiri mkubwa kwa sasa hapa nchini.
“Kupitia
kampeni hii, Coca-Cola itaweza kuwaletea simulizi zaidi juu ya
mafanikio ya watu ambao hawakukata tamaa licha ya kutofanikiwa mara
kadhaa katika safari zao za kuelekea kwenye mafanikio. Sababu
zilizowafanya wasikate tamaa ni kutokana na imani yao kuwa kuna siku
ambayo wangekuja kufanikiwa. Na hicho ndicho tunachotaka vijana wa
Kitanzania waweze kuiga. Wawe na moyo wa kutokata tama licha ya
kukumbana na changamoto nyingi katika safari yao kuelekea katika
mafanikio,” Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka.
Coca-Cola
imewekeza katika programu ya soka kwa vijana ijulikanayo kama Copa
Coca-Cola ambapo vipaji vya wachezaji nyota kama vile Thomas Ulimwengu
anayecheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya nchini Congo na
mfungaji bora wa ligi kuu nchini Simon Msuva anaechezea Yanga vimeweza
kuibuliwa na Copa Coca-Cola. Vile vile Coca-Cola inasaidiia kuinua
wanamuziki wa Tanzania kupitia programu ya Coke Studio.
0 comments :
Post a Comment