Pichani
ni muonekano wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania ndani ya
Karume Hall katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’,
ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Pichani ni wananchi wakitembelea banda hilo na kupata taarifa
mbalimbali za shughuli za Umoja huo nchini Tanzania.(Picha zote na
Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akitoa maelezo kwa mwananchi katika picha za viongozi mbalimbali
waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa Shirika la Umoja Mtaifa duniani ambalo
hivi sasa linaongozwa na Ban Ki-Moon.
Pichani
juu na chini ni Ismael Mnikite (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini kwa
wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya 39
ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K
Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (katikati) akifafanua jambo kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji
Steven (kushoto) aliyetaka kujua zaidi kuhusiana na ushiriki wa Umoja wa
Mataifa katika tatizo la ajira za vijana nchini. Kulia ni Emmanuel
Johnson kutoka Shirika la Afya (WHO) nchini.
Ismael
Mnikite (kulia) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC),
akitoa darasa la Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDG's)
yanayotekelezwa na nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania
ikiwa ni miongoni mwa nchi wananchama kwa mmoja wa wananchi
aliyetembelea banda hilo lililopo Karume Hall katika maonyesho ya
Sabsaba.
Emmanuel
Johnson (kulia) kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) nchini akitoa
maelezo ya ripoti ya UNDAP kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji Steven
alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya
Sabasaba lililopo Karume Hall.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) na Salome Mwambinga (wa pili kulia) kutoka (IAEA)
wakihudumia wananchi waliotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini Dar.
Wananchi wakisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa.
Wananchi wakijichukulia vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Na Modewjiblog team
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu, amesema tangu Umoja huo ulipotoa fursa kwa wananchi wanaotembelea
maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya sabasaba kutoa maoni kuhushu
utendaji wake hapa nchini mpaka sasa zaidi ya watu 600 wameshiriki kutoa
maoni yao.
Amesema
watu waliotoa maoni hapo wametumia njia tofauti ikiwemo mtandao, ujumbe
mfupi wa maandishi (sms), njia ya mdomo na kwa kuandika katika fomu
maalum zinazopatikana katika banda lao
Bi.
Temu amewashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao na kuwataka
kuendelea kutoa ushirikiano pia katika mambo mbalimbali ikiwemo miradi
ya maendeleo inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa nchini.
Jinsi
ya kuendelea kushiriki kutoa maoni kwa njia ya ujumbe mfupi wa
maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa
watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453,
kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa
Vodacom ni namba 15055 bila makato yoyote kwenye simu yako.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
0 comments :
Post a Comment