Askari wa kikosi cha bendera kutoka JWTZ wakiwa kwenye mazoezi.
Askari wa JWTZ wakionesha mfano wa kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu.
Vikosi vya JWTZ na FFU wakionesha ukakamavu.(P.T)
Eneo maalumu la mnara ambalo shughuli zote za mashujaa wetu zitaonyeshwa siku hiyo.
Kamanda wa paredi (hayupo) akitoa amri kwa askari kushusha silaha.
Kamanda wa paredi ambaye haonekani pichani akiwashitua askari, HEY!
Kikosi cha Bigura kikitoa heshima.
Askari wa JKT wakitoka nje ya uwanja baada ya kumaliza mazoezi.
Askari wa kikosi maalum kutoka Magereza wakitoka nje ya uwanja baada ya kumaliza maandalizi.
KATIKA
kuelekea kwenye tukio muhimu la kuwakumbuka maofisa na wapiganaji wa
vita Tanzania ambalo hufanyika kila mwaka ifikapo Julai 25, maandalizi
yamekamilika ambapo leo baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa
katika mazoezi ya mwisho ndani ya Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja
jijini Dar.
Maadhimisho
hayo ya siku ya mashujaa yanatarajiwa kupambwa na matukio mbalimbali
ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Dokta Jakaya Mrisho kikwete ambaye itakuwa ni mara
yake ya mwisho kuhudhuria tukio la namna hiyo akiwa madarakani.
Pia
sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuiriwa na wazee mashuhuri waliopigana
vita. Wageni wengine ni mabalozi kutoka nchi mbalimbali.
Pichani juu ni baadhi ya vyombo vya usalama nchini vikifanya maandalizi ya mwisho.
HABARI/PICHA: DENIS MTIMA NA HARUNI SANCHAWA/GPL


0 comments :
Post a Comment