Saturday, July 11, 2015
Nkupamah blog
Mambo yamezua jambo ambapo wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu inayokutana hivisasa chini Rais Dkt Jakaya Kikwete wameonesha wazi kupinga uamuzi wa mbunge wa Monduli Edward Lowassa jina lake kukatwa.
Hayo
yamedhihirika hivisasa wakati Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt Jakaya
Kikwete akiingia kufungua mkutano huo ambapo imezoeleka wajumbe huimba
kuwa na imani na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dkt Jakaya Kikwete lakini leo
hali imekuwa tofauti.
Wajumbe walipaza sauti zao wakiimba wimbo wa kuwa na imani na Edward Lowassa.( Tuna Imani na Lowassa...!!! Tuna Imani na Lowassa!!)
Wajumbe walipaza sauti zao wakiimba wimbo wa kuwa na imani na Edward Lowassa.( Tuna Imani na Lowassa...!!! Tuna Imani na Lowassa!!)
Mkutano
huo wenye wajumbe 324 kati ya 374 umehudhuriwa na wajumbe mbalimbali
wakiwemo baadhi ya wanasiasa walio omba ridhaa ya kuteuliwa kugombea
urais ndani ya chama hicho.
Kwa
upande mwingine mtia nia aliyechujwa Prof. Mark Mwandosya yeye kwa
upande wake amewashukuru wananchi kwa ushirikiano walio mpa na
kusisitiza kuwa hatogombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Mmoja wa watia nia CCM Samweli Sitta.
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa katika mkutano wa Halmashauri kuu CCM.
Polisi katika jengo la makao makuu CCM hivisasa.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment