Saturday, July 11, 2015
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumkaribisha Kikwete kufungua mkutano huo. Kushoto ni Dk. Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto_ alipoingia ukumbini. Waliosimama mbele ni Wajumbe waalikwa wa kikao hicho kutoka Baraza la Ushauri la Wazee Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa na wengine ni Makamu Wenyeviti wastaafu Mzee John Malecela na Mzee Pius Msekwa
Kikao hicho kikiendelea
YALIYOJIRI KABLA YA KIKAO HICHO
Aliyekuwa
muomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameenguliwa,
Edward Lowassa akiwasili kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM
kuhudhuria kikao cha NEC.Lowassa akiingia ukumbini
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Mzee Msidai akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho cha NEC
Mjumbe wa NEC, Dk. Chegeni akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, wa CCM, Zakiah Megji akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Steven Wasira akifuatwa na Waandishi wakati akiingiaukumbini
Kada wa CCM kutoka Zanzibar, Mohamed Raza akizungumza na waandishi ambapo aliipongeza Kamati Kuu ya CCM kwa kuweza kufanya uteuzi wa watu watano na kueleza kuwa inabidi waliokosa kuteuliwa wawe watulivu kwa kuwa ndiyo Demokrasia
Muomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Bernard Membe ambaye amefanikiwa kuingia tano bora, akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho leo
Muomba kuteuliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameingia tano bora, John Magufuli, akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa NEC, aliyekuwa akimnong'oneza jambo kabla ya kuingia ukumbini
Waomba kuteuliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM ambao wamefanikiwa kuingia tano bora, Januari Makamba na John Magufuli wakicheka kwa furaha walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kuingia kwenye kikao hicho.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Januari Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora walipokuwa nje ya ukumbi wakati wa kikao hicho
Wakuu wa vyombo vya habari vya CCM, Angel Akilimali (Uhuru FM) na Ramadhani Mkoma (Uhuru Publications Ltd
Muomba ridhaa ya CCM kuwania Urais Bernard Membe akiwasalimia wajumbe ukumbini pengine kuomba kura zao kabla ya kuanza kikao hicho
Waomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, ambao wamefanikiwa kuingia tano bora Bernard Membe na Dk. Asha Rose Migiro wakisalimiana ukumbini wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Samwel Sitta ambaye pia aliomba nafasi hiyo lakini hakuingia tano bora
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Lazaro Nyalandu ambaye hakuingia tano bora, akizungumza na Adam Malima
Wajumbe wakiwa ukumbini
"Usijali kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwigulu Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
"Usijali kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwigulu Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Edward Lowassa ambaye hakupita tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
"Naomba kura yako Ndugu yangu, tena napiga magoti" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
January Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa wakati wa kikao hicho cha NEC
Membe na Januari Makamba wakisalimiana ukumbini
Baadhi ya wajumbe ukumbini
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mzee Sitta wakati wa kikao hicho cha NEC
Dk. Asha-Rose Migiro ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa na kumuomba kura wakati wa kikao hicho cha NEC leo
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti wakiwa kwenye kikao hicho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kikao hicho cha NEC
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika jengo la White House baada ya baadhi ya walioomba ridhaa ya CCM kuwania urais na kutoingia tano bora, kudaiwa kuandaa fujo wakati wa kikao hicho cha NEC. Picha zote na Bashir Nkoromo
0 comments :
Post a Comment