Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi
wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM
Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya
Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja
kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa
Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose
Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January
Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu
yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie
atakuwa Mgombea Urais.
Posted by Nkupamah blog
Posted by Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment