Obama awazima wengi kwa kukutana na Ruto
Obama awazima wengi kwa kukutana na Ruto
Takriban
saa ishirini hivi tangu rais wa Marekani Barack Obama awasili nchini
Kenya swala ibuka limekuwa, Je atakutana na naibu rais wa Kenya bwana
William Ruto au la ?
Naibu rais Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Kesi dhidi yake inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague Uholanzi.
Wadadisi
wa maswala ya kidiplomasia walikuwa wamebashiri kuwa rais Obama
asingelikutana naye na ima atafanya hivyo itakuwa mkutano wa kisiri wala
hakutakuwa picha yoyote kwani Ruto angali anatazamwa kama mshukiwa wa
makosa jinai.
Ruto
Wakati huohuo , Bwana Ruto amenukuliwa mara kadhaa akikashifu hadharani swala la mapenzi ya jinsia moja.
Yamkini
majuma kadhaa yaliyopita, Ruto, alitangaza wazi kuwa, atapinga shinikizo
za aina yoyote kutoka kwa serikali ya Rais Obama ya kutaka Kenya
ihalalishe na kuwatambua watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kulikuwa na dhana kuwa msimamo huo ungemfanya kutofautiana na rais Obama lakini hilo sasa limezikwa katika kaburi la sahau.
Na alipowasili katika ikulu ya Nairobi alipokewa kwa taadhima kuu ya amiri mkuu wa jeshi na kupigiwa mizinga 21 ya heshima.
Hata hivyo hii leo Naibu Rais wa Kenya, William Ruto ameamkuana na Rais Barrack Obama katika ikulu ya rais nchini Kenya.
William Ruto
Ingawa ni
salamu tu, kati ya Obama na Ruto, tendo hilo limekuwa na umuhimu mkubwa
nchini Kenya na kuashiria uhusiano ulioko kati ya Kenya na Marekani.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao hawangekutana kutokana na kesi inayomkabili Ruto katika mahakama ya uhalifu ya ICC.
Ruto
hakuwa katika wageni waliompokea Rais Obama alipotua nchini Kenya na
tukio hilo lilichangia uvumi kuwa Ruto hangekutana na rais Obama.
Baadhi ya
vyombo vya habari nchini Kenya viliripoti kuwa Ruto hangeruhusiwa
kukutana na Obama kwani ni mshukiwa kwa kuhusika katika vurugu za baada
ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini ambapo watu elfu moja waliuwawa na
maelfu kuachwa bila makao.
Rutoo
Hata
hivyo Rais Uhuru Kenyatta alieleza awali kuwa Obama atakutana na
Serikali ya Kenya na Ruto ni mmoja wa viongozi wakuu katika serikali
hiyo.
Kauli
hiyo ilitiliwa mkazo na waziri wa nchi za nje, Amina Mohammed kwenye
mahojiano ya kipekee na BBC aliposema kuwa hakuna sababu zitakazomzuia
Ruto kukutana na Rais Obama.
Aidha,
Ruto amekuwa katika mstari wa mbele kupinga ndoa kati ya watu wa jinsia
moja na kueleza kuwa Kenya haitahalalisha ndoa za aina hizo.
0 comments :
Post a Comment