- Written by Nkupamah log
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea wakati wa ufunguzi
wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa
iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi na Kushoto ni Mwenyekiti
msaidizi soka la vijana wa TFF Khalid Abdallah.
Mkurugenzi
wa ufundi wa TFF Salim Madadi akiongea wakati wa wa semina elekezi ya
Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo (Julai 7,
2015) jijini Dar es Salaam. Katikati Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania
Jackson Mmbando akifatiwa na Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub
Nyenzi.
Viongozi
soka kutoka katika mikoa inayoshiriki michuano ya Airtel wakifatilia
Seminar elekezi ya Michuano ya Airtel Rising Stars iliyofanyika
iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Mikoa
inayoshiriki katika michuano ya mwaka huu ni pamoja na ya Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa wasichana huku
mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and Arusha ikiwa ni
kwa upande wa wasichana.
Mwenyekiti
soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa
Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars iliyoshirikisha
wasimamizi na viongozi wa mikoa itakayoshiriki katika michuano ya Airtel
Rsing Stars inayotegemea kutimua vumbi 20 Julai. Kushoto ni Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando na kulia ni baadhi ya
viongozi wa TFF.
Shirikisho
la Soka nchini (TFF), limewasisitiza viongozi wa soka ngazi za mikoa
kutambua kuwa lengo kuu la michuano ya Airtel Rising chini ya vijana wa
miaka 17, ni kuibua vijana kwa manufaa ya Taifa kwa baadaye na sio
kulelekeza nguvu zao katika kupata matokeo mazuri uwanjani kama ambavyo
watu wengi hufikiri.
“Tumegundua
kwamba baadhi ya viongozi wa soka mikoani wana fikra tofauti na lengo
la michuano hii, wao huangalia zaidi kupata matokeo mazuri uwanjani
kuliko kutafuta vijana wenye vipaji kama lilivyo lengo la michuano hii.
Na hii ndio sababu kuu ya ongezeko la tatizo la watu kuleta vijana
waliozidi umri uliolengwa katika program hii”, amesema.
Mwesigwa
amemimina pongezi kwa kampuni ya Airtel nchini kwa kuamua kuwekeza
katika soka hapa nchini hasa la vijana. “ Michuano ya Airtel Rising
Stars imekuwa ni chachu kubwa hasa kwa upande wa soka la wanawake,
ambapo idadi kubwa ya wachezaji wanatokana na progamu hii”, amesema
Mwesigwa.
Ameongeza
kuwa soka la vijana limekuwa ni njia ya uhakika na endelevu katika
maendeleo ya soka hapa nchini. “Kwa mfano nchi ya Cameroon, wamepata
mafanikio makubwa na ya kuvutia kutokana na kuwekeza katika program za
vijana”, alisema, huku akiiongeza pia Hisapania kama nchini nyingine
ambayo ilifanya hivyo na kufanikiwa kuchukua kombe la dunia.
Mwesigwa
amewataka viongozi wa soka ngazi mbalimbali nchini kufuata taratibu na
kanuni za michuano hii. “Nataka muelewe kuwa hii ni program muhimu na
nyeti sana kwa taifa, kwa sababu inalenga hasa vijana ambao wanahitaji
uangalizi wa karibu sana ili kutimiza ndoto zao.
Kama
ukiwafundisha kuwatii waamuzi, basi watafanya hivyo katika kipindi
chote cha maisha yao ya soka, na endapo ukiwafundisha kutowatii waamuzi
basi pia watafanya vivyo hivyo,”alisema huku akiwaonya vikali viongozi
kutowapandikiza wachezaji imani za kishirikina.
Michuano
hiyo imepanga kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya awali (mikoa) julai
20 na kuhitimishwa Agusti 30, ambapo ngazi ya taifa itaanza Septemba 11
hadi 21 jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Aitel
nchini Jackson Mmbando amesema kuwa hii ni fursa nyingine tena adhimu
kwa vijana kuonesha vipaji vyao ambavyo vitawawezesha kutimiza malengo
yao ya baadaye kupitia mchezo wa soka.
Airtel
Rising Stars mwaka huu inaenda bega kwa bega na kampeni mpya
inayojulikana kwa jina la ‘It’s Now’ huku nahodha wa Ivory Coast ambaye
pia ni kiungo wa Manchester City Yaya Toure akiongoza kampeni hiyo.
Kampeni hii inalenga kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia nyanja
mbalimbali kama vile michezo, mtindo wa maisha na mziki lakini vilevile
kuwapa mbinu zitazaowawezesha kupata ufumbuzi wa masuala ya
kiteknolojia na kuona fursa zinazowazunguka.
Michuano
ya Airtel Rising Stars mwaka huu itajumuisha mikoa ya Mwanza, Morogoro,
Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa wasichana huku mikoa ya
Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and Arusha ikiwa ni kwa upande
wa wasichana
0 comments :
Post a Comment