Mwandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura (katikati) akisoma jina la mwananchi aliyehitajika kwenda kujiandikisha.
Wananchi wakisubiri kujiandikisha eneo la kituo cha Kijitonyama-Mpakani B.
Hapa wananchi wakitafakari hatma yao ya kujiandikisha. (P.T)
Mwananchi
aliyekwenda kujiandikisha (kulia) akipigwa picha na kamera maalum kwa
ajili ya kupata kitambulisho eneo la Sinza- Mori, Dar.
Waandikishaji wa BVR wakiwa katika mashine za za kuandikishia.
Wananchi
waliojitokeza nje ya geti la Shule ya Msingi Sinza-Maalum kwa ajili ya
kuanza kujiandikisha huku ndani wananchi walioandikishwa majina yao jana
wakipatiwa huduma ya kuandikishwa.
Mwananchi aliyekwenda kujiandikisha (kulia) akiweka vidole kwenye mashine ya kuchukua alama za vidole eneo la Mlimani City, Dar.
Mama
mmoja, mkazi wa Sinza A akisaidiwa na mwandikishaji jinsi ya kukaa ili
aweze kupigwa picha kwa ajili ya kitambulisho cha kupigia kura.
....akipigwa picha.
Wananchi wakiwa katika foleni kusubiria kujiandikisha maeneo ya Mlimani City, Dar.
IKIWA
sasa ni siku ya tatu tangu zoezi la uandikishaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura uanze kwa teknolojia ya Biometric Voters Regitration
(BVR), hali imezidi tete baada ya wakazi wa Dar kupata usumbufu wa
kuamka asubuhi na mapema kwenda kujiandikisha na kurudi bila mafanikio.
Mapema
hii leo mwandishi wetu amefanikiwa kutembelea baadhi ya vituo kama vya
Sinza, Shule ya Msingi Mapambano, Mwenge, Kijitonyama pamoja na maeneo
ya Mlimani City Dar na kushuhudia umati mkubwa ukiwa kwenye foleni kwa
ajili ya kujiandikisha.
Katika
baadhi ya vituo hivyo, zoezi lilionekana likiendelea vizuri huku baadhi
ya maeneo yakiwa na changamoto za wananchi kulalamikia ubovu ‘Solar
power’ zinazotumika katika mitambo ya uandikishaji kuwa jua linapopungua
na mitambo husimama kutokufanya kazi.
Kituo Cha
Kijitonyama-Mpakani B, maeneo ya Mori wananchi wengi wamelalamikia
foleni kuwa ndefu na zoezi kwenda taratibu, huku wakilalamikia suala la
kuandikishwa majina kisha kupatiwa vitambulisho siku inayofuata.
“Tunaomba
waandikishaji wa BVR wasilaze majina kwa kuwa inasababisha msongamano
na vurugu kwa wananchi wanaojitokeza siku inayofuata tena wakiwa
wameamka alfajiri kushinda vituoni hapo,” alisema Amina Suleiman, mkazi
wa Sinza-Mori jijini Dar.
Aidha,
kwa upande wa waandikishaji nao wamelalamikia wananchi kwa kutozingatia
taarifa zinazotelewa juu ya changamoto za kwenda kujiandikisha wakiwa
wamejipaka mafuta mikononi hatua inayosababisha mashine kutofanya kazi
vizuri.
Waandikishaji
hao pia wamezungumzia suala la wananchi kutokuwa wavumilivu katika
changamoto hizo wanazokutana nazo pindi wanapokwenda kujiandikisha, hasa
pale wanapotumia lugha za kuudhi na kuwataka kuwa wavumilivu.
HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL


0 comments :
Post a Comment