26 July 2015
Mgombea
nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Wema Sepetu,
akisindikizwa kwa maandamano kuelekea ukumbi wa mkutano wa kanisa la
katoliki mjini Singida, kushiriki zoezi la uchaguzi wa kuchagua wana CCM
wawili watakaoshika nafasi za ubunge viti maalum.
Mgombea
nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Wema Sepetu, akiwa na
na mgombea mwenzake Sara Mwambu, wakipokelewa kwenye lango la kuingilia
kwenye ukumbi wa mkutano wa kanisa la katoliki mjini Singida, kwa
ajili ya kushiriki uchaguzi huo.Wakati Wema alishika nafasi ya nne kwa
kupata kura 90, mwenzake Sara, alishika nafasi ya tano kwa kupata kura
47.
Mshindi
wa kwanza wa ubunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Aysharose Ndogholi
Mattembe (kulia) na mshindi wa pili, Martha Mosses Mlata, waakiwashukuru
wapiga kura kwa kuwapa ridhaa ya kuwa wabunge wa viti maalum mkoa wa
Singida kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kanisa
katoliki mjini hapa.
Mgombea
ubunge viti maalum kupitia CCM Wema Sepetu, akiwashukuru wapiga kura wa
UWT mkoa wa Singida kwa waliompa kura 90 na wale pia ambao hawakumpa,
kwa madai kwamba wote kwa pamoja wamemhamasisha kuanza safari yake ya
kisiasa.
Mpiga picha wa magazeti ya Mwananchi, Mwananchi jumapili, The Citizen na Sunday citizen na mwanaspotinews@yahoo.co.uk,
Leah Samike na msanii wa filamu nchini,Wema Sepetu (kulia) wakati
kwenye ukumbi wa mikutano kanisa katoliki,muda mfupi kabla hawajaanza
kunadi sera zao ili waweze kuchaguliwa kushika nafasi mbili za ubunge
viti maalum mkoa wa Singida kupitia CCM.
Baadhi
ya wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jumuiya ya umoja wa wanawake
Tanzania (UWT) mkoa wa Singida, walioshiriki uchaguzi mkuu wa kuchagua
wabunge wawili wa viti maalum mkoa wa Singida.Mkurugenzi wa the British
School ya Zanzibar, Aysharose Ndoghili Mattembe, alikuwa mshindi wa
kwanza kwa kuzoa kura 318 kati ya 940 zilizopigwa.Mshindi wa pili Martha
Mosses Mlata,alipata kura 325.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MSANII
maarufu wa tasnia ya filamu nchini, Wema Isaac Sepetu, ametangaza rasmi
kuwa safari yake ya kuwatumikia wakazi wa mkoa wa Singida kupitia
siasa, imeanza rasmi.
Wema
ametangaza azima yake hiyo, muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo
ya uchaguzi wa waombaji wa ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida
uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Kanisa la mjini hapa.
Wema
ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro hicho
alipata kura 90 na kushika nafasi ya nne kati ya waombaji 13, wakati
Mbunge wa viti maalum kwa vipindi vitatu mfululizo , Diana Mkumbo
Chilolo, aliapishwa baada ya kuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 182.
Msanii
huyo ambaye alifanya vizuri katika kujinadi, alisema amejifunza mengi
na kubaini mapungufu mbalimbali yaliyochangiwa na ugeni wake katika
siasa,na kwamba kuanzia sasa anajipanga vizuri, ili aweze kufanya
vizuri zaidi kwenye safari yake ya kisiasa.
“Nitumie
nafasi hii kuwashukuru wale walionipa kura 90 na wale wote
walioninyima kura kwa ujumla wao,wamenipa hamasa na ari kubwa kuanza
rasmi safari yangu ya kisiasa, Ninachoomba ni Mungu aendelee kunipa
uzima, ili siku moja ndoto yangu hii, iweze kutimia”,alisema Wema huku
akitabasamu.
Awali
mapema Wema alipofika Ofisi ya CCM mkoa, alikuwa kivutio kikubwa na
kila mwana CCM alijitahidi kupiga picha naye huku wakisahau kambi zao za
uchaguzi.
Alipoanza
safari ya kuelekea ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki mahali
palipofanyikia mkutano wa uchaguzi, aliandamana na kikundi cha burudani
cha Ikungi, na alishangiliwa na watu wengi waliojitokeza kando kando ya
barabara kwa ajili ya kumwona.
Aidha,aadhi
ya wajumbe walidai kwamba kama kujinadi kwa mgombea ingekuwa sifa pekee
ya mgombea kushinda ubunge wa viti maalum, Wema angepata angeshinda
nafasi hiyo.
Wamedai
kwamba Wema alijinadi vizuri, kwa ufasaha mkubwa na kwa ufupi na
kuvuta hisia za wajumbe ambao walishindwa kujizuia na kuvunja kanuni kwa
kumpigia makofi msanii huyo.
0 comments :
Post a Comment