Afisa Utamaduni Mila na Desturi
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Elizabeth Hizza aliyesimama kulia akiongea na
baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni
iliyopo jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa mila na Desturi nzuri za
Mtanzania.
(Picha na Benjamin Sawe – WHVUM).
Mkurugenzi Msaidizi Lugha, Idara
ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Hajjat Shani Kitogo aliyenyoosha mikono akiongea na baadhi ya
wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini
Dar es Salaam wakati
timu ya Wizara ilipotembelea shule hiyo kufanya
utafiti kuhusu Majina Fiche.Majina Fiche ni majina yanayotolewa kwa njia
ya mafumbo baada ya kutokea kisa au mkasa Fulani kwa jamii ikiwa na
lengo la kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na lugha za jamii.
Afisa Utamaduni Mila na Desturi
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. Boniface Kadili akiongea na baadhi ya wanafunzi
wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es
Salaam juu ya umuhimu wa mila na Desturi nzuri za Mtanzania.
Afisa Utamaduni Lugha Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Christopher Mhongole akiongea na baadhi ya wanafunzi wa
darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es Salaam
juu ya umuhimu wa kuwa na Majina Fiche katika jamii ikiwa ni juhudi za
kukuza mila na desturi za Mtanzania.
Mkurugenzi Msaidizi Mila na
Desturi Bi. Lily Beleko akiongea na baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es Salaam kuhusu
umuhimu na nafasi ya Kiswahili katika kujiletea maendeleo.
0 comments :
Post a Comment