Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkoani Manyara,Mkuu wa Mkoa
Mh.Joel Bendera akiwasili katika viwanja vya Halmshauri ya Mji wa Mbulu
akiongozana toka kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa –Bw.Ally Uledi, Mkurugenzi
wa CHF Bw.Eugene Mikongoti na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dr.Michael
Kadeghe.
Mkurugenzi
wa CHF Bw.Eugene Mikongoti akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika
moja ya banda la maonyesho ambapo wananchi walipata fursa ya kupimwa
afya zao, kuchangia damu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zihusuzo
CHF iliyoboreshwa na NHIF.Wengine toka kushoto ni Bw.Isaya Shekifu Kaimu
Meneja wa NHIF – Manyara, Bw. Ally Uledi- Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Manyara na Dr.Heri Marwa Mkurugenzi wa Mradi wa Health Insurance –
PharmAcess Tanzania.
Mh.Mary
Nagu –Waziri katika ofisi ya Raisi Mauhusiano na Uratibu na Mbunge wa
Hanang akawaelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na CHF ILIYOBORESHWA
katika siku ya uzinduzi .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa shirika la
PharmAccess kutoka Uholanzi Bw.Sicco Van Gelder ambao ndio wafadhili wa
mradi huu wakishirikiana na NHIF.
Mgeni
rasmi wa siku ya uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkuu wa Mkoa wa Manyara
Mh.Joel Bendera akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe
kukabidhi moja ya pikipiki tano zilizotolewa kwa maafisa wa CHF
iliyoboreshwa ili kuwarahisishia kazi ya uandikishaji na uhamasishaji
kwa wananchi wa tarafa tano za wilaya ya Mbulu.
Mkuu
wa mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiwasha moja ya pikipiki tano
alizokabidhi kwa maafisa wanaoshughulika na CHF ILIYOBORESHWA mbele ya
umati wa wananchi wa wilaya ya Mbulu katika siku ya uzinduzi wa mradi
huu kimkoa.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera akimkabidhi kadi ya CHF
iliyoboreshwa mwanachama mpya aliyejiunga katika siku ya uzinduzi wa
kimkoa wilayani Mbulu mkoani Manyara.
---
Anna Makange, Mbulu.
Mkuu
wa mkoa wa Manyara, Mh. Joel Bendera amezindua rasmi Mfuko wa Afya ya
Jamii Uliboreshwa (iCHF) mkoani Manyara.Uzinduzi huo uliohudhuriwa na
wageni mbalimbali akiwemo Mh.Mary Nagu (Mbunge - Hanang) na Waziri
katika ofisi ya Raisi Mahusiano na Uratibu, Wakuu wa wilaya za Hanang na
Mbulu pamoja Wawakilishi wa wizara ya afya na Ustawi wa Jamii,
ulifanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Mbulu. Mkuu wa Mkoa
alitoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha kuwa
wanasimamia vizuri mradi huu na kuhamasisha wananchi wajiunge kwa wingi
ili kufanikisha sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya kwa
wananchi wote.
Pia
halmshauri za wilaya mkoani Manyara zimetakiwa kuweka bajeti maalum
itakayowezesha utekelezaji wa mpango endelevu wa kuziingiza kaya maskini
katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kila mwaka ili kuwahakikishia
huduma bora za matibabu.
Mradi
huo wa iCHF mkoani Manyara unaendeshwa kwa ushirikiano baina shirika la
Pharm Access International (PIA) la Uholanzi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya(NHIF) na Halmashauri za wilaya za Mbulu, Babati na Hanang kwa
lengo la kuboresha huduma na kuhamasisha idadi kubwa ya wananchi
kujiunga na mfumo wa kulipia kabla gharama za matibabu ili kuzuia vifo
visivyo vya lazima katika jamii.
Bendera
alisema ili kuiwezesha serikali kufikia lengo lake la kufikisha huduma
bora za afya kwa kila mtanzania kuna umuhimu wa kipekee kwa halmashauri
zinazounda mkoa huo kuhakikisha wananchi wote wanajisajili katika iCHF
wakiwemo maskini ili nao waweze kuhakikishiwa upatikanaji wa matibabu.
“Kwa
kutambua changamoto ya kutokuwepo rasilimali za kutosha katika vituo
vya kutolea huduma ndio maana serikali iliamua kuanzisha mfumo huu wa
kuchangia kidogo kila mwaka gharama za matibabu kabla ili kumwezesha
kila mwananchi kupata matibabu kwa nia ya kuchangia fedha kidogo.”,
alisema.
Aidha
aliongeza, “Wito wangu kwenu wananchi ni jiandikisheni kwa wingi
kwasababu ugonjwa haupigi hodi… kwa upande wa halmashauri hebu anzeni
kuweka fedha kwa mpango mtakaokubaliana ili wale maskini nao waweze
kusaidiwa kupata matibabu kama wenzao wengine wenye uwezo wa kuchangia”,
alisema.
Awali
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Eugine Mikongoti akizungumza katika uzinduzi huo aliwataka watoa huduma
za afya kupitia iCHF kumaliza malalamiko ya wagonjwa kwa kuhakikisha
michango yote ya wananchi inatumika ipasavyo kwa ajili ya kununulia dawa
na vifaa tiba ili kuwawezesha kuona thamani halisi ya fedha zao.
0 comments :
Post a Comment