Maneja
wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank
Madebwe(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and
Agriculture” iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na
masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake
ya kilimo klabu,Kushoto ni Doris Chaula na Faraja Alex ambao ni
washiriki wa semina hiyo.
Mkulima
wa Mkoa wa Arusha Faraja Alex(kulia)aliyeshiriki katika semina ya
Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu
masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture”akisalimiana na
Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank
Madebwe(katikati)wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika
mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Anayeshuhudia
kushoto ni mshiriki wa semina hiyo Doris Chaula.
MWenyekiti
wa Taasisi ya AMSHA,Biubwa Ibrahimu(katikati)akimsikiliza jambo maneja
wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(kushoto)
wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture”
iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya
kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo
klabu,Kulia ni mshiriki wa semina hiyo Faraja Alex.
Washiriki
wa semina ya Vijana iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and
Agriculture” Bi. Doris Chaula na Faraja Alex(kulia)wakimsikiliza jambo
Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank
Madebwe(katikati)wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika
mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu.
Zaidi
ya vijana 1000 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walihudhuria katika
semina ya kupambana na wimbi kubwa la ajira.Semina hiyo iliyoandaliwa
na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na kuhuthuriwa na zaidi
vijana 1000 ilikuwa na kauli mbiu isemayo “Kilimo Biashara Ndio Mpango
Mzima”-Agribusiness is the real deal na vijana wengi walitoa mawazo yao
na kuelezwa fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya kilimo na jinsi
gani zinaweza kuwakwamua kiuchumi na kujiajiri wao wenyewe baadhi ya
sekta hizo zikiwa za ufugaji,upandaji wa miti,kilimo cha kisasa na jinsi
ya kusindika mazao na kuyapeleka kwenye masoko.
Akiongea
kwa niaba ya washiriki wenzake Bw.Jason Kato ambaye ni mhitimu wa Chuo
Kikuu alisema kuwa semina kama hizi ni muhimu kuwafikia wananchi wengi
na kuwafungua akili kujua kuwa kilimo ndio silaha pekee ya kuondoa
tatizo la ajira nchini hususani kwa vijana badala ya kufikiria kuwa
kilimo sio kazi au ni kazi ya watu walioshindwa maisha.
Naye
Meneja wa huduma ya Kilimo Klabu inayotolewa na Vodacom Tanzania,
Bw.Frank Madembwe alibainisha kwamba huduma ya matumizi ya teknolojia ya
simu ya mkononi inayotolewa na kampuni yake imeelezwa kuwa imeanza
kuonyesha mafanikio makubwa na ni silaha ambayo itaondoa umaskini nchini
kupitia sekta ya kilimo iwapo itatumika ipasavyo.
Hayo
yamebainishwa na Meneja huyo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa
na Taasisi ya Vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini na
kushirikisha mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali
yanayoshughulika na kilimo na kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Bw.Medembwe
alisema kuwa kutokana na matumizi ya simu za mkononi kuongezeka
nchini,Vodacom ikiwa ni kampuni inayoongoza kuwa na mtandao mkubwa
nchini iliona umuhimu wa kubuni huduma za kurahisisha maisha ya
watanzania ambao wengi ni wakulima wanaoishi vijijini na ndio kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali ikaibuka na huduma ya kilimo Klub.
Alisema
ndani ya Kilimo Klub kuna huduma mbalimbali zinazopatikana ambazo
zimerahisisha maisha ya wakulima ambazo ni M-Pesa,huduma ambayo imeleta
ukombozi kwa kurahisisha utumaji fedha na upokeaji fedha bila kusahau
kufanya mihamala mbalimbali ya Malipo pia ipo huduma ya M-Pawa
inayowezesha mtumiaji wake kujiwekea akiba kupitia simu yake ya mkononi
na Kujipatia mkopo wenye masharti nafuu .
Aidha
madembwe alisema ipo huduma ya M-Kopa inayowawezesha wakulima hususani
sehemu ambazo hazijafikiwa umeme kupata nishati hiyo kwa kupatiwa vifaa
vya umeme unaotumia jua kwa mkopo na unafuu wa bei pia kuna huduma ya
Sokoni inayowawezesha wakulima kupata taarifa za bei za mazao.
“Kupitia
Kilimo Klub tunaamini kuwa mabadiliko makubwa yatatokea katika sekta ya
kilimo kuanzia kwa wakulima wenye mpaka kwa wanunuzi wa mazao ya
wakulima na hii inadhihirisha kuwa teknolojia ikitumika ipasavyo inaweza
kuleta mabadiliko makubwa kama ambavyo tumeanza kushuhudia”.Alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya MKURABITA ambaye alikuwa mgeni
rasmi Bi.Serapia Mgembe alisifu jitidaza zinazofanywa na taasisi
mbalimbali hususani zinazoshughulika na kuinua wakulima nchini kwa kuwa
bado kuna fursa nyingi kwenye sekta hiyo na aliwataka vijana
kuchangamkia kilimo biashara ili kuboresha maisha yao.
Taasisi
nyingine ambazo zilizowaoa vijana kuhusu kilimo zilishoshiriki semina
hiyo ni Agri pro Focus,ANSAF,AMSHA, na Tanzania Graduates Farmers
Association,pia kulikuwepo na maonyesho ya mazao ya kilimo kutoka
vikundi vya kilimo na usindikaji wa mazao ambapo pia washiriki waliweza
kupata maelezo jinsi huduma ya M-Kopa inavyotolewa kupitia mitandao wa
Vodacom na vituo vya mawakala wake.
0 comments :
Post a Comment