Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
(kulia), akisalimiana na Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus
Bahati mara baada ya kuwasili Bohari Kuu ya Maji wakati wa ziara yake ya
siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar
es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar
es Salaam (DAWASA) ambapo aliitimisha ziara hiyo Agosti 27, 2015
kwakukagua miradi iliyopo daraja la mpiji na Kerege na maungio ya maji
ya wazo.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya
Bohari Kuu ya maji iliyoko Boko jijini Dar es Salaam wakati ziara yake
ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es
Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es
Salaam (DAWASA).
Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya
Maji, Datus Bahati akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi za Bohari Kuu
ya Maji kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (hayupo pichani).
Kushoto
ni Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi
,Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati (kulia) pamoja na
Wakandarasi wa miradi hiyo na maofisa kutoka Wizara ya maji na waandishi
wa habari wakimskiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati
akizungumza (hayupo pichani).
Baadhi
ya waandishi wa habari (wakwanza pembeni) wakimsikiliza kwa umakini
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati akizungumza.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa
Bohari Mkuu wa Wizara ya Maji, Crepn Balamu, jinsi mita za kisasa kutoka
Uturuk zinavyofanya kazi ambapo amesema kazi yao ni kuingiza na
kuwauzia mamlaka za maji katika miji nchini, kushoto ni Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula.
Kutoka
kulia ni Bohari Mkuu wa Wizara ya Maji, Crepn Balamu akimpa maelezo
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla vifaa vya kuunganisha maji wakati wa
ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa
wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa
wa Dar es Salaam (DAWASA)
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla na ummbe wake wakishuudia maungio mapya ya
maji yaliopo Kerege Bagamoyo mbapo yamekamilika kwa asimilia 95.wakati
wa ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika
mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA)
Wakiangali maungio ya maji katika mto Mpiji Bunju.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na ujumbe wake wakiwasili katika eneo la Wazo tayari kuangalia maungio ya maji.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla na ujumbe wake wakiangalia maungio ya maji
katika eneo la wazo jijini Dar es Salaam Agosti 27, 2015 wakati wa
ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa
wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa
wa Dar es Salaam (DAWASA).
SIKU YA PILI YA ZIARA
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
na ujumbe wake wakiwa katika eneo Kigamboni jijini Dar es Salaam katika
visima vya Kimbiji na Mpera.akizungumza baada ya kutembelea maeneo hayo
ambapo alisema ameridhishwa na uchimbaji wa visima hivyo visima 6
vimekamilika bado 14 kati ya visima 20 vinavyotakiwa katika mradi
huo.Waziri alikuwa katika ziara yake ya siku ya pili Agosti 26, 2015 .
Akipata maelezo mara baada ya kufika katika kisima kilichokamilika cha Kisarawe 11 chenye urefu wa mita 415.
Hapa wakijionea mashine ya usafishaji wa kisima eneo la Kisarawe 6 kilichochimbwa kwa urefu wa mita 473.
Picha zote na Alex John.
0 comments :
Post a Comment