Naibu
Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo
juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo
alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia
vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya
NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Vifaa
mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya
NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimuonyesha Katibu
Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka moja ya vifaa
vilivyowasili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.
Naibu
Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka juu ya NEC
inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea
kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali
vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha
Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni Kulia ni Mkurugenzi wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw Kailima Ramadhani.
Serikali
imeahidi kuipatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi fedha zote ambazo
inazihitaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kuelekea Uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu kutoka vyanzo vyote vya
mapata.
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka amesema hayo leo
alipo itembelea Tume ya Tafifa ya Uchaguzi kuona maandalizi ya Uchaguzi
Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na
Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari.
"Changamoto ya kifedha ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa
ikikabiliana nayo awali sasa haipo tena kwakuwa serikali imedhamiria
kuipa NEC fedha zote ambazo inazihitaji katika kuhakikisha Uchaguzi mkuu
unafanyika Octoba 25 mwaka huu.
Fedha hizo zitatolewa kwa awamu, kutokana na ratiba ya tume ikiwa ni
pamoja na ununuzi wa vifaa ambavyo vimeanza kuwasili , mafunzo kwa
wasimamizi wa Uchaguzi na zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani,
Wabunge na Rais.
Vifaa vilivyo wasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na
vitutuli[vibanda vya kupigia kura], mabango [yanayo onesha kituo cha
kupigia kura.
0 comments :
Post a Comment