Bwana Pollard anasema kuwa anataka kuhamia Israel kwa sababu mkewe anaishi huko.
Viongozi wa Israel wamekuwa wakifanya kila juhudi kuishinikiza serikali ya Marekani kumwachilia Pollard kutoka gerezani.
Afisa wa ujasusi wa Marekani aliyehukumiwa kwa kupatikana na hatia ya
kufanyia ujasusi Israel ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kutumikia
kifungo cha miaka 30.
Jonathan Pollard, aliyekuwa wakati mmoja afisa wa maswala ya usalama
katika jeshi la wanamaji la Marekani alipatikana akiuzia maafisa wa
Israel nyaraka za siri za Marekani mwaka 1985.
Chini ya masharti ya kauchiliwa kwake, hapaswi kuondoka Marekani kwa muda wa miaka mitano baada ya kuachiliwa.
0 comments :
Post a Comment