Image copyrightAFPImage captionPolisi wa Mali wameingia katika hoteli hiyo
Maafisa wa serikali ya Mali wamesema sasa hakuna mateka wowote
waliosalia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako iliyokuwa
imeshambulia asubuhi na watu wenye silaha huku miili ya watu 18 ikidaiwa
kupatikana ndani ya hoteli hiyo.
Waziri wa usalama wa Mali Salif Traore ameambia kikao cha wanahabari
kwamba watu wenye silaha walioshambulia hoteli ya Radisson kwa sasa
hawazuilii mateka wowote.
Afisi ya rais wa Mali imeandika kwenye Twitter ikishukuru maafisa wa
usalama na mataifa yaliyosaidia kukabiliana na shambulio hoteli hiyo ya
kifahari.
Watu watatu wamethibitishwa kufariki na wanajeshi wawili kujeruhiwa.
Ubelgiji imesema afisa mmoja wa serikali yake ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo.
Geoffrey Dieudonne alikuwa Mali kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa serikali.
Uvamizi huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa mapema asubuhi kwenye hoteli
hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.
Image copyrightRadisson Blu HotelImage captionTovuti ya hoteli hiyo inaieleza kama "hoteli ya kifahari"
Baadhi ya ripoti zilisema watu walioshambulia hoteli hiyo huenda wakafika 10.
Moja kwa Moja: Shambulio hotelini Bamako
Ufaransa ambayo imekuwa na wanajeshi Mali tangu 2013 ilituma wanajeshi
wake kusaidiana na wanajeshi wa Mali. Aidha, polisi maalum wapatao 50
walitumwa kutoka Paris.
Kundi la wapiganaji wa kijihadi la al-Murabitoun limedai kuhusika kwenye
shambulio hilo kupitia ujumbe kwenye akaunti ya Twitter ya kundi hilo,
kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ingawa habari hizo
hazijathibitishwa. Kundi la Al-Murabitoun linajumuisha makundi mawili
ambayo yalijitenga kutoka kwa tawi moja la al-Qaeda eneo la Afrika
Kaskazini.
Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13, wakiwemo wafanyakazi
watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu katika mji wa Sevare,
katikati mwa Mali.
Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba
unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala
salama nao raia wawasiliane na familia.
0 comments :
Post a Comment