Tuesday, December 1, 2015
@nkupamah blog
Agizo
la Rais Dk. John Magufuli kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kodi
nchini, limeanza kuwa mwiba baada ya mabasi ya Kampuni ya Usafirishaji
Dar es Salaam (UDA), kukamatwa kutokana na kukwepa kodi.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Richard Kayombo, jana alisema mabasi tisa ya UDA yalikamatwa kutokana na
kukiuka sheria za mlipakodi.
Mbali
na UDA, Kayombo alisema TRA pia iliyakamata mabasi ya kampuni nyingine
kutokana na kushindwa kulipa kodi ambapo walitumia kampuni ya udalali ya
Majembe Auction Mart.
Kayombo
alisema operesheni ya TRA kuwakamata wafanyabiashara wanaokwepa kodi ni
endelevu nchi nzima na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa
wanaokaidi kutekeleza sheria.
Hata
hivyo, Kayombo hakutaka kuzungumzia kwa undani kuhusu kiwango cha kodi
ambacho hakikulipwa na UDA, akidai kuwa hiyo ni siri ya mlipakodi na
mamlaka yenyewe.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa UDA, Robert Kisena, alithibitisha kukamatwa
kwa mabasi yake ambayo alisema uzembe huo ulifanywa na idara yake ya
uhasibu.
Kisena alisema muda wa kulipia kodi ulikuwa umefika, lakini idara yake ya uhasibu haikuweza kulipa viwango vinavyotakiwa.
“Ni
kweli kuna magari yetu matatu au manne yamekamatwa na tatizo kubwa ni
kodi ya magari, ambayo tulijua mtu wetu wa uhasibu amelipa, lakini kumbe
alikuwa hajalipa,” alisema Kisena huku akisisitiza kuwa taratibu za
kuyakomboa magari hayo zimefanyika ambapo wamekwishalipia gharama
zilizokuwa zinahitajika.
0 comments :
Post a Comment